Wananchi wa Zambia wanapiga kura kwenye uchaguzi wa kihistoria
.
Wananchi wa Zambia wanapiga kura Alhamisi hii,
katika uchaguzi ambao ulikumbwa na vurugu za hapa na pale kati ya wafuasi wa
vyama viwili vikubwa vinavyopewa nafasi, chama tawala cha PF na wale wa
upinzani wa UPND.
Ikiwa ni miezi 18 tu imepita toka Rais Edgar
Lungu ashinde kwenye uchaguzi ambao ushindi wake ulikuwa finyu, yeye pamoja na
mpinzani wake wa karibu Hakainde Hichilema, wanakutana tena kwenye
kinyang'anyiro kingine, ambapo wagombea 9 wanashiriki.
Kura elfu 27 pakee ndizo zilizowatenganisha
wagombea hawa kwenye uchaguzi uliofanyika mwaka 2015.
Watu watatu wameripotiwa kuuawa wakati wa
kampeni, huku vurugu za mara kwa mara zikishuhudiwa kati ya wafuasi wa chama
tawala cha PF cha Rais Edgar Lungu na wale wa upinzani wa chama cha UPND wa
Hakainde Hichilema.
Kuelekea uchaguzi wa Alhamisi, Agosti 11, tume
ya taifa ya uchaguzi nchini Zambia, ilitoa taarifa kwa uma, ikikosoa vurugu
ambazo zimeshuhudiwa, huku ikisema kuwa zimetia doa hali ya amani na utulivu
pamoja na demokrasia iliyokuwa imeshamiri kwenye taifa hilo.
Mwezi uliopita, kampeni zililazimika
kusitishwa kwa muda wa siku kumi katika jiji la Lusaka, baada ya kutokea
makabiliano makali kati ya wafuasi wa chama tawala cha PF na wale wa UPND.DRThe Post Zambia
Hata hivyo vurugu bado zimeshuhudiwa hata
wakati wa zoezi lenyewe la kupiga kura kwenye baadhi ya maeneo ya nchi, huku
siku ya Jumatano, wafuasi wa upinzani wakijikuta pabaya wakati mgombwa wao
alipokuwa akihitimisha kampeni.
Mabadiliko yaliyofanyika hivi karibuni,
yanamaanisha kuwa mshindi wa kinyang'anyiro hiki ni lazima apate zaidi ya
asilimia 50 ya kura zote, vinginevyo watalazimika kwenda kwenye duru ya pili ya
uchaguzi.
Wachambuzi wa mambo wanasema kuwa uchaguzi huu
ni wa kwanza kuwa na shinikizo kubwa za wafuasi wa pande mbili, ambapo mchuano
unatarajiwa kuwa mkali huku wengi wakishindwa kubashiri hali ya mambo
itakavyokuwa licha ya upinzani kupewa nafasi.

Comments
Post a Comment