Vijana wajadili jinsi ya kushiriki kufanikisha SDGs
Wiki hii, kuanzia tarehe 10 hadi 12 Agosti, ambayo ni Siku ya
Kimataifa ya Vijana, vijana kutoka sehemu mbalimbali duniani wamekusanyika hapa
kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa kwenye jukwaa linalowezesha mazungumzo
na kuibua ubia baina ya vijana wenye umahiri mkubwa, maafisa waandamizi wa
Umoja wa Mataifa, sekta binafsi na asasi za kiraia.
Baraza hilo la vijana lilimulika hasa jinsi ya kuwezesha vijana
walio uongozini na vijana waliobobea katika taaluma mbali mbali, ili washiriki
kikamilifu katika utekelezaji wa Ajenda ya Umoja wa Mataifa ya 2030 kuhusu
maendeleo endelevu. Kwa mengi zaidi kuhusu Baraza hilo la vijana, ungana na
Joshua Mmali katika makala ifuatayo.

Comments
Post a Comment