Amani na maendeleo mada kuu kwenye umHamishia
Uhusiano baina ya amani, ujenzi wa amani na maendeleo endelevu
umemulikwa kwenye mkutano wa pamoja wa Baraza la Umoja wa Mataifa la
Kiuchumi na Kijamii na Tume ya Ujenzi wa Amani. Priscilla Lecomte na taarifa
kamili
Akihutubia mkutano huo, Naibu Katibu Mkuu Jan Eliasson amesema
kwamba, ili kudumisha amani, ni muhimu kuingiza suala hilo katika miradi ya
maendeleo, kabla mizozo haijaibuka, akikumbusha kwamba mara nyingi mizizi ya
mizozo ni sababu za kiuchumi na kijamii.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Kudumu wa Kenya kwenye Umoja wa
Mataifa Macharia Kamau, ambaye pia ni mwenyekiti wa Tume ya Ujenzi wa amani
aliyeongoza mkutano huo, amesisitiza kwamba suala la ujenzi wa amani ni suala
mtambuka katika ajenda ya maendeleo endelevu.
(sauti ya Balozi Kamau)
"Tukizungumza kuhusu ujenzi wa
amani, tukizungumza kuhusu amani, tunazungumza kuhusu ajenda nzima ya 2030.
Nimezungumza pia kuhusu umuhimu wa utawala wa sheria kwa sababu hakuna nchi
ambayo inaweza kudumisha amani bila taasisi imara iliyojengwa kwa kuheshimu
utawala wa sheria."
Sambaza

Comments
Post a Comment