Matangazo yanayowalenga watoto yadhibitiswe:Wataalam UN
Katika kuelekea Siku ya Kimataifa ya Vijana hapo Ijumaa
Agosti 12, wataalamu wawili wa Umoja wa mataifa kuhusu haki za binadamu,
wameonya kuhusu athari za matangazo ya biashara yanayowalenga watoto wadogo.
Wataalamu hao huru, Juan Pablo Bohoslavsky, anayehusika na
madeni ya nje na haki za binadamu na mwakilishi maalumu kuhusu haki ya afya Dainius
Püras, wamesema matangazo hayo ni yale yanayowajengea watoto utamaduni wa
matumizi ya kupindukia na hulka ya madeni, na wamezitaka serikali kote duniani
kudhibiti matangazo yanayowalenga watoto moja kwa moja.
Wamesema ujumbe wa biashara una uwezo wa kujenga tabia ya
watoto ya muda mrefu katika muktada wa matumizi na masuala ya fedha.
Wameongeza
kuwa pia matangazo hayo yanaweza kusababisha tabia isiyo bora kwa watoto
wangali wadogo na akuathiri maisha yao ya baadaye, hasa katika kununu vitu
ambavyo si vya lazima bila kujali athari za muda mrefu za kifedha na kiafya,
kama vyakula vyenye kiwango kikubwa cha sukali au mafuta

Comments
Post a Comment