Ban ziarani California; SDGs na wakimbizi kwenye ajenda


Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, yupo ziarani Los Angeles, jimbo la Kalifonia, Marekani, ambako anatarajiwa kukutana na viongozi katika fani ya sanaa ya muziki na filamu, ili kujadili jinsi wanavyoweza kuunga mkono malengo ya Umoja wa Mataifa.
Katika ziara hiyo, Ban anatarajiwa pia kukutana na Mwenyekiti wa Kamati ya masuala ya kigeni katika bunge la Marekani, Ed Royce.
Aidha, Katibu Mkuu anatarajiwa kushiriki hafla ya kuwapatia makazi mapya wakimbizi, hafla ambayo imeandaliwa na mashirika ya International Rescue Committee (IRC) na Annenberg Foundation.


Comments

Popular posts from this blog

VYOMBO VYA HABARI VINAWAJIBU WA KUELIMISHA JUU YA MALENGO 17 YA MAENDELEO ENDELEVU

DINI YAELEZWA KUWA KICHOCHEO CHA KUTIMIZA SDGS

7 hatua kuelekea maendeleo endelevu ifikapo mwaka 2030