Bado hakuna usawa baina ya weusi na wazungu Afrika Kusini:Kamati
Kamati
ya Umoja wa Mataifa dhidi ya utesaji imekamilisha kujadili ripoti ya Afrika ya
Kusini kuhusu utekelezaji wa mkataba wa kimataifa wa utokomezaji wa mifumo yote
ya ubaguzi wa rangi. Flora Nducha na maelezo kamili.
Akiwasilisha
ripoti hiyo Naibu Waziri wa Sheria na Maendeleo ya Katiba wa Afrika ya
Kusini, John Jeffery amesema kukata mizizi ya ubaguzi wa rangi nchini humo ni
zaidi ya kufuta sheria za ubaguzi wa rangi na kuzibadilisha na zile za kuleta
usawa na utawala wa sheria.
Amesema
kufanikisha hilo kunahitaji utashi wa kisiasa , rasilimali, ujenzi wa taasisi
mpya za kuunga mkono demokrasia na kuendelea kutambua mtazamo wa kitaifa wa
haki za kijamii na kiuchumi kwa wote. Hata hivyo amesema hatua zimepigwa katika
kujaribu kuinua hali ya maisha ya kila raia .
“Kwa hivyo tunatoa tamko madhubuti ya kuwa Afrika Kusini ni taifa
la watu wa aina mbili, watu weupe wenye mafanikio makubwa katika maisha bila
kujali jinsia yao na jeographia, na lingine lililokua kubwa zaidi ni la watu
weusi walio masikini na waathirika wakubwa ni wanawake wa mashinani.”
Nayo
kamati imeitaka serikali ya nchi hiyo kuhakikisha hatua inazochukua zinakwenda
sanjari na mikataba ya haki ya kimataifa na mapendekezo ya kamati dhidi ya
utesaji, ikiongeza kuwa, bado kuna ubaguzi wa wazi baina ya weusi walio wengi
na wazungu wachache nchini humo. Pia ikitaja hofu yake kuhusu ongezeko la chuki
dhidi ya wageni, na hali ya kutovumiliana.

Comments
Post a Comment