USHIRIKA MZURI BAINA YA SAYANSI NA SERA UNAHITAJIKA KUFIKIA SDG'S-RIPOTI
Katibu
mkuu akiwa na wafanayakazi wa kujitolwa mjini Vienna wakiwa na mabango ya
SDGs.(Picha:UM/Nikoleta Haffar)
Uelewa wa misingi ya kisayansi
katika kuchukua hatua utahitajika ili kufikia malengo ya maendeleo endelevu
SDG's ifikapo mwaka 2030 imesema ripoti mpya iliyotolewa leo na Umoja wa
mataifa wakati wa kongamano la ngazi ya juu kuhusu maendeleo endelevu.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo ya 2016 ya
SDG's vipengee muhimu kwa ajenda ya mwaka 2030 kama kitahitajika nini
kuhakikisha kwamba hakuna atakayesalia nyuma , bado hilo halijatafitiwa
kisayansi.

Ripoti imebaini kwamba ajenda mpya inahitaji kuuliza maswali tofauti tofauti na mengi hayana majibu ya kitafiti.
Ripoti imebaini kwamba ajenda mpya inahitaji kuuliza maswali tofauti tofauti na mengi hayana majibu ya kitafiti.
Ripoti hiyo iliyojikita kwenye
tathimini ya kisayansi zaidi katika kufikia malengo ya maendeleo endelevu,
imeandaliwa na idara ya Umoja wa Mataifa ya uchumi na maendeleo ya kijamii na
imejumuisha utaalamu wa kiufundi wa wanasayansi na wataalamu 245.
Ripoti imesisitiza ni muhimu kutambua
ni nani aliyeachwa nyuma, hasa watu masikini, wasiojumuishwa,wanaobaguliwa na
wasiotendewa usawa ili sera za kuzuia hayo ziweze kuwekwa.

Comments
Post a Comment