UNECE, UNITAR ZAANZISHA UBIA WA KUTEKELEZA SDGS
Katika kuwezesha utekelezaji wa
malengo ya maendeleo endelevu SDGs, taasisi mbili za Umoja wa Mataifa mjini
Geneva zimeanzisha ubia ili kukuza viwango na uwezo katika kufikia melengo
hayo.
Taasisi hizo ambazo ni kamisheni ya
uchumi ya bara Ulaya UNECE na taasisi ya mafunzo na utafiti UNITAR kwa
pamoja katika taarifa zimeeleza kuwa maeneo yatakayopewa kipaumbele
katika jitihada za pamoja ni ubia katika taasisi binafsi za umma, usalama
barabarani na mazingira.
Taarifa hiyo inasema kuwa
utekelezaji wa SDGs unakabiliwa na changamoto kadhaa, mathalani uwezeshaji
kifedha kwa ajili ya miundombinu mipya ya maji safi, afya, na upatikanaji wa
nishati ambavyo vinahitaji takribani dola bilioni saba kwa mwaka.
Zikitolea mfano, taasisi hizo
zimesema serikali hususani zile za kipato kidogo ambapo mahitaji ni ya dharura
hazitakuwa na rasilimali fedha za kutosha kuziba pengo hilo licha ya misaada ya
kimaendeleo. Hivyo ushirikiano wa sekta binafsi na uwezeshaji mkubwa wa kifedha
utahitajika.

Comments
Post a Comment