madhara ya tumbaku mwilini
Mwili wa mvutaji tumbaku
Kila sekunde nane, mtu mmoja hufariki
kutokana na utumizi wa tumbako.
Imebainika kuwa saba kati ya wavutaji sigara kumi, huanza uraibu
huu wakiwa wangali watoto. Wanaoendelea kuvuta sigara kwa muda mrefu hufupisha
maisha yao kwa miaka 20 hadi 25. Sababu ni kuwa sigara ina kemikali zaidi ya
4,000 ambazo zina uwezo wa kudhhuru afya ya binadamu. Madhara yanayosababishwa
na uvutaji sigara ni mengi na yamesambaa mwilini kote. Yafuatayo ni baadhi tu
ya maradhi yatokanayo na utumiaji wa tumbako.
1.Kung’oka
kwa nywele
Uvutaji sigara hudhoofisha kinga ya mwili na
kisha kudhuru mizizi ya nywele . hii husababisha kung’oka kwa nywele mapema.
2.Magonjwa
ya macho
Wavutaji sigara hupata magonjwa ya macho mara
nyingi kuliko wasiovuta. Sehemu ya macho inayopitisha mwangaza inaweza kufichwa
kama vile wingu linavyoficha jua(yaani kwa ikimombo) na kusababisha upofu.
Ugonjwa huu husababishwa kwa njia mbili. Kwanza moshi wa sigara huwasha macho
na pili kemikali zilizo ndani ya sigara hupita kwenye mishipa , damu na
hatimaye kudhuru macho. Sigara pia husababisha kudhoofika kwa sehemu ya kati ya
macho(retina) na hivyo
kupunguza uwezo wa macho kuona vizuri na hata kutofautisha rangi(macular
degeneration).
3.Kukunjana
kwa ngozi
Kemikali zinazopatikana ndani ya sigara
hupunguza uwezo wa ngozi kujirekebisha hivi basi ngozi huzeeka haraka na
kupoteza uwezo wa kulainika. Mvutaji wa sigara huonekana mzeee zaidi kuliko
umri wake haswa.
4.Magonjwa
ya masikio
Uvutaji sigara huleta magonjwa mengi ya
masikio . Sababu ni kwamba uvutaji wa sigara husababisha uchafu kuganda kwenye
mishipa ya damu na hivyo kupunguza mwendo wa damu hadi kwenye sehemu za ndani
za masikio. Moshi na kemikali za tumbako pia hujeruhi sehemu za ndani za
masikio na majeraha hayo yanaweza kuambukiza hata ubongo(menengitis). Yote haya yanaweza kusababisha uziwi.
5.Saratani
ya ngozi
Uvutaji sigara unasababisha saratani ya
ngozi. Kemikali za sigara husababisha vidonda kwenye ngozi na ambavyo haviponi
kwa urahisi. Baada ya muda hugeuka kuwa saratani.
6.Magonjwa
ya meno
Sigara hutatiza mdomo na kuongeza uchafu
unaoganda kwenye meno hivi kusababisha kuoza kwa meno, harufu mbaya mdomoni na
uchafu wa meno. Sigara pia hutatiza kupona kwa vidonda hasa baada ya kung’olewa
kwa jino. Saratani ya mdomo na ulimi inapatikana zaidi kwa wavutaji sigara na
watumiaji wa tumbako za aina nyingine.
7.Magonjwa
ya mapafu
Uvutaji wa siagara ndio sababu kubwa zaidi ya
saratani ya mapafu. Pia husababisha kupasuka kwa vibofu vya hewa safi na kutoa
harufu mbaya mwilini. Wavutaji pia hupata saratani ya koromeo na kuziba njia ya
hewa na hivo basi inabidi kutobolewa kwa kishimo kwenye shingo hili kuwezesha
mwadhiriwa kupumua.
8.Mifupa
Sigara inasababisha mifupa kuwa myepesi na
kupunguza nguvu. Sababu ni kuwa kemikali zilizoko ndani ya sigara hupunguza
uwezo wa mwili kujenga mifupa iliyo na nguvu. Mifupa kama hii huvunjika kwa
urahisi na kuchukua muda mrefu sana(asilimia 80 zaidi ya mifupa ya kawaida)kupona.
9.Ugonjwa
wa moyo
Sigara ndio sababu kubwa zaidi ya magonjwa ya
moyo. Inasababisha moyo kupiga kwa kasi zaidi na hivyo kuongeza msukumo wa damu
mwililni( high
blood pressure). Mwishowe husababisha mshtuko wa moyo na
hata kifo.Moja kati ya kila vifo tatu ulimwenguni hutokana na magonjwa ya moyo
na huua zaidi ya watu milioni moja kwenye nchi za Afrika.
10.Vidonda
vya tumboni
Sigara hupunguza uwezo wa mwili kujikinga
dhidi ya viini vinavvyosababisha vidonda tumboni. Pia hupunguza uwezo wa tumbo
kustahimili nguvu ya asidi baada ya kula. Vidonda vya mvutaji basi huwa ni
vigumu kutibu, na mara nyingi hutokea tena baada ya kupona.
11.Vidole
Kutu ya sigara hukusanyika na kuganda kwenye
kucha na vidole vya mvutaji. Kisha hubadilisha rangi ya vidole na kucha kuwa za
manjano au maji ya kunde. Ngozi ya vidole pia hukauka na kuwa ngumu sababu ya
joto na kemikali za sigara.
12.Wanawake
Sigara huongeza hatari ya kupata saratani ya
fuko la uzazi(cancer of theuterus ).
NI vigumu zaidi kwa mwanamke mvutaji sigara kutungwa mimba na ni rahisi sana
kwake kumpoteza mtoto katika mimba.(miscarrige).
Uvutaji wa sigara pia humfanya mwanamke kumzaa mtoto aliyekufa(stillbirth) au aliye na uzito
usiotimia wa kawaida. Watoto hawa huwa na afya duni baadaye. Sababu ni kuwa
kemikali za sigara hupunguza mwendo wa mtoto kukua akiwa angali mimbani. Sigara
pia husababisha ugumba(menopause)
kabla ya wakati wake. Sigara pia inaweza kumfanya mwanamke kuwa tasa.
13.Wanaume
Sigara inapunguza mpigo wa damu kwenye sehemu
za uume. Sigara pia huharibu mbegu za wanaume na kwa hiyo watoto wanaowazalisha
huwa na uwezekano mkubwa zaidi wa kupata magonjwa ya saratani. Sigara pia huwafanya
wanaume kuwa tasa.
14.Magonjwa
ya ngozi
Sigara huleta magonjwa mengi ya ngozi kama
vile uvimbe, kuwashwawashwa na hudhoofisha hali ya ngozi.
15.Ugonjwa
wa ‘Buerger’
Huu ni ugonjwa wa uvimbe kwenye mishipa ya
damu ya miguuni na mikononi. Mishipa hii huzibika na kuzuia mwendo wa damu
kwenye sehemu zilizoathirika. Isipotibiwa kwa haraka,mvutaji anaweza kukatwa
miguu au mikono.
16.Saratani
Zaidi ya kemikali 40 zinazopatikana kwenye
tumbako zimethibitishwa kusababisha saratani.
Ukilinganisha na asiyevuta sigara :
16(a).Mapafu
Mvutaji ana uwezekano wa mara 22 zaidi wa
kupata saratani ya mapafu
16(b).Pua
Mvutaji ana uwezekano wa mara 2 zaidi kupata
saratani ya pua.
16(c).Ulimi
Mvutaji ana uwezekano wa mara 2 zaidi kupata
saratani ya ulimi.
16(d).Tumbo
Mvutaji ana uwezekano wa kupata saratani ya
tumbo mara 3 zaidi.
16(e).Figo
Mvutaji ana uwezekano wa kupata saratani ya
figo mara 5 zaidi.
Saratani
Zinginezo
Uchunguzi unaonyesha kuwa saratani ya mdomo ni
hadi mara 27, koo(mara 12), koromeo(mara10).Uchunguzi pia umebaini kuwa kuna
uhusiano fulani kati ya uvutaji sigara na saratani ya matiti

Comments
Post a Comment