UNICEF na ombi la dola Bilioni 2.8 kukwamua watoto maeneo mbali mbali



Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limezindua ombi la dola Bilioni 2.8 kwa ajili ya kufikia watoto Milioni 43 wanaokumbwa na dharura mbali mbali duniani.

Kwa mara ya kwanza asilimia 25 ya ombi hilo, kiasi ambacho ni kikubwa zaidi kitaelekezwa kwenye elimu kwa watoto walio kwenye majanga ambapo nusu yao ni wale wa Syria walioko nchini mwao nan chi jirani.
Mkurugenzi wa UNICEF anayehusika na miradi ya dharura Afshan Khan amesema mamilioni ya watoto wameporwa haki yao ya elimu kutokana mizozo licha ya kwamba elimu ni zana ya kuokoa maisha na kujenga mustakhabali bora wa maisha  yao.
Ombi la sasa ni maradufu ikilinganishwa na miaka mitatu iliyopita ambapo UNICEF imesema chanzo kikubwa ni mizozo na mabadiliko ya hali ya hewa ambayo yanasababisha watoto kukosa elimu.
Kiasi kingine cha fedha ambacho ni zaidi ya dola Milioni 30 zitaelekezwa kusaidia janga la wakimbizi na wahamiaji Ulaya huku dola Milioni 25.5 zikilenga watoto nchini Burundi waliosaka hifadhi Rwanda na Tanzania.
Pesa hizo zitakazokusanywa na UNICEF zitatumika kwa mara moja kwa maeneo tajwa na nyingine kwa ajili ya dharura zinazoweza kuibuka.


Comments

Popular posts from this blog

VYOMBO VYA HABARI VINAWAJIBU WA KUELIMISHA JUU YA MALENGO 17 YA MAENDELEO ENDELEVU

DINI YAELEZWA KUWA KICHOCHEO CHA KUTIMIZA SDGS

7 hatua kuelekea maendeleo endelevu ifikapo mwaka 2030