Mawaziri wa mazingira kutoka kote duniani wanakutana Nairobi Kenya kwa ajili ya maandalizi ya baraza kuu la Umoja wa mataifa la mazingira UNEA kutathimini na kutoa taswira ya sera za kimataifa za mazingira.

Wajumbe wamejadili uwezekano wa mada zitakazojadiliwa kwenye UNEA ,mkutano wa ngazi ya juu kabisa wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kufanya maamuzi ya mazingira. Taasisi ya UNEA inaundwa na wawakilishi Zaidi ya 25 kutoka nchi 10 ikiwemo mawaziri na manaibu waziri wa mazingira.
Mkutano wa pili wa baraza kuu la Umoja wa mataifa la mazingira ,UNEA utafanyika mwezi Mai mwaka huu na wa kwanza ulifanyika mwaka 2014 mwezi June ikiwaleta pamoja wawakilishi kutoka mataifa 163 wakiwemo mawaziri Zaidi ya 100. Wawakilishi hao walijadili masuala ya maendeleo endelevu (SDG's), ajenda ya maendeleo baada yam waka 2015 na pia walipitisha maazimio 16.

Comments

Popular posts from this blog

VYOMBO VYA HABARI VINAWAJIBU WA KUELIMISHA JUU YA MALENGO 17 YA MAENDELEO ENDELEVU

DINI YAELEZWA KUWA KICHOCHEO CHA KUTIMIZA SDGS

7 hatua kuelekea maendeleo endelevu ifikapo mwaka 2030