Maendeleo Endelevu 17 ya Dunia yazinduliwa Tanzania
UMOJA wa Mataifa kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania wamezindua rasmi malengo ya MaenEndelevu 17 ( SDGs).
Malengo
hayo ambayo pia yanajulikana kama malengo ya dunia yamezinduliwa jana
Septemba 29 katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
Uzinduzi
huo ulifanywa na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi
Mkazi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez, Kamishina wa mipango (POPC) Bw.
Paul Kessy, na Kamishina wa Mipango wa Zanzibar, Bw. Ahmed Makame kwa
niaba ya serikali, Bi. Fionnuala Gilsenan, Balozi wa Ireland na Bi. Liz
Lloyd, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered Tanzania kwa
niaba ya wadau wa mradi wa Project Everyone Partners.
SDGs
ni wito wa dunia wa kuchukuliwa kwa hatua za kuufuta umaskini, kuihami
dunia dhidi ya uharibifu wa mazingira na kuhakikisha kwamba kila
mwanadamu anaishi maisha stahiki katika amani na ustawi.
Katika
malengo hayo 17 yapo makusudio 169 yanayotoa ramani ya utengenezaji wa
sera za maendeleo na namna ya kutekeleza kwa miaka 15 ijayo.

Comments
Post a Comment