Vijana wataka sauti yao isikike katika Umoja wa Mataifa
Vijana kutoka maeneo mbalimbali ya dunia wameuomba Umoja wa Mataifa usikilize kauli zao wakati wa uundwaji wa ajenda ya maendeleo ya baada ya mwaka 2015.
Wawakilishi wa vijana kutoka Afrika wamekutana leo mjini New York ili kujadili ushirikishwaji wa vijana kutoka ukanda huo, kwenye jukwaa la vijana linalomalizika leo katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa. Balozi wa Shirika la maskauti wa kike duniani, Yvonne Akoth, ameiambia Redio ya Umoja wa Mataifa matarajio yake.
Sauti ya Yvonne.
Aidha mwakilishi huyo kutoka Kenya amesema ushirikiano wa vijana katika utungaji sera na maamuzi ya mamlaka za serikali umeimarika nchini mwake.
Sauti ya Yvonne.

Comments
Post a Comment