Watu milioni 2 wakosa maji machafuko yakishika kasi Aleppo- UNICEF
Watu milioni mbili wameachwa bila fursa ya maji ya bomba, wakati mashambulizi na mapigano yakiharibu mtandao wa umeme ulio muhimu kwa ajili ya kusukuma maji kwenye mabomba ya mji mzima wa Aleppo, Syria.
Mashambulizi ya tarehe 31 Julai yaliharibu transfoma ya umeme, na ongezeko la mapigano limefanya kuwa vigumu kukarabati nyaya za mtambo huo, na hivyo kusababisha mji mzima kukosa maji kwa siku nne sasa.
Kwa mujibu wa Hanaa Singer, mwakilishi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto (UNICEF) nchini Syria, watoto na familia zao Aleppo wanakabiliwa na hali mbaya, na kwamba maji hayawezi kusubiri, akitoa wito kwa pande zote kutoa fursa ya mafundi kufanya ukarabati. Christophe Boulierac ni msemaji wa UNICEF.

Comments
Post a Comment