Mabadiliko ya mapigo ya moyo ni ya hatari kwa wanawake zaidi kuliko wanaume
Mabadiliko ya mapigo ya moyo ni ya
hatari kwa wanawake zaidi kuliko wanaume, kwa mujibu wa tafiti 30 ,
zilizohusisha zaidi ya wagonjwa milioni nne.
Kwa mujibu wa utafiti huo wanawake
wenye mapigo ya moyo yanayobadilika badilika (AF) walikuwa na uwezekano wa kufa
kwa maradhi ya moyo ama kiharusi mara mbili zaidi.
Wanawake mara nyingi hawaponi vizuri
kwa dawa za kudhibiti mabadiliko ya mapigo ya moyo ama hupatikana na maradhi ya
moyo baadae kuliko wanaume.
"Uwezekano mmoja ni kwamba
wanawake wenye mapigo ya moyo yanayobadilika hawatibiwi ipasavyo ikilinganishwa
na wanaume ," Connor Emdin na wenzake ,katika chuo kikuu cha Oxford,
walieleza.
Wakati huo huo, wataalam wanasema
madaktari hawanabudi kuelewa kuhusu uchunguzi huu ili kuepuka vifo vinavyoweza
kuzuiwa.
Image caption Takrban watu milioni
moja wanatatizo la mabadiliko ya mapigo ya moyo nchini Uingereza
Takriban watu milioni moja nchini
Uingereza wana mapigo ya moyo yanayobadilika.
Unaweza kujichunguza mwenyewe ikiwa
una tatizo hilo kwa kuhisi mapigo yako kwa sekunda 30.
Ni jambo la kawaida kuhisi
mabadiliko ya mapigo ya moyo mara chache , mfano kukosa kwa pigo moja, kukosa
kwa pigo moja ama mapigo zaidi, ni jambo la kawaida si jambo la kukutia hofu .
Image copyright SOUTHERN ILLINOIS
UNIVERSITYSCIENCE PHOTO LIBRARY Image caption Mapigo ya moyo ya kazi kubwa
yanaweza kusababisha uchovu na kupungua kwa pumzi
Lakini ikiwa ikiwa utahisi mapigo ya
moyo yatabadilika kwa kipindi kirefu , unapaswa kumuona daktari.
Mapigo pia yanaweza kuwa ya kasi
sana , zaidi ya mapigo 100 kwa dakika unapokua umetulia husababisha uchovu na
kupungua kwa pumzi.
Dawa zinaweza kudhibiti hali hii na
kuzuia hatari ya kiharusi (kuganda kwa damu ama kuvuja kwa damu kwenye ubongo).


Comments
Post a Comment